Hali ya kiutu Ukanda wa Gaza inaendelea kuwa mbaya
5 Desemba 2023Matangazo
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema mateso ya watu wa Gaza 'hayavumiliki' na kutoa wito wa kuwepo suluhisho la kisiasa na kuhakikisha raia wanalindwa kwa mujibu wa sheria za vita na kuruhusu misaada kuingia Gazabila vikwazo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema karibu watu milioni 1.9 ikiwa ni sawa na asilimia 80 ya wakazi wote huko Gaza wameyakimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7.