1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Jeshi la Israel lauwa Wapalestina 9 huko Ukingo wa Magharibi

22 Februari 2023

Vikosi vya Israel vimewauwa Wapalestina tisa, wakiwemo watatu waliojihami kwa silaha, raia watatu, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 90, katika Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4NqMa
Westjordanland | Razzia Israelischer Streitkräfte in Nablus
Picha: Raneen Sawafta/REUTERS

Watu walioshuhudia na madaktari wamesema kuwa mauaji hayo yamefanyika katika operesheni iliyoendeshwa kwenye eneo tete, lenye kukaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Kwa upande wake jeshi la Israel limethibitisha kufanya operesheni zake katika mji wa Nablus, lakini halikutoa taarifa zaidi kuhusu maafa yaliyotokea.

Vyanzo kutoka upande wa Palestina vinasema makamanda wawili wa kundi linalojiita Islamic Jihad waliuawa pamoja na mtu mwingine aliyekuwa kajihami kwa silaha. 

Neblus na mji wa karibu wa Jenin inalengwa na operesheni za kijeshi, ambazo zimekuwa zikiongezeka kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, tangu yalipotokea mashambulizi ya Wapalestina. 

Wizara ya Afya wa Palestina inasema kwa mwaka huu pekee Wapalestina 57, wakiwemo wenye kujihami kwa silaha pamoja na raia, wameauwa.