1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Waziri mkuu Tony Blair kukutana na Mahmoud Abbas na Ehud Olmert

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiY

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anatarajiwa kukutana hii leo na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert pamoja na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas katika juhudi za kutafuta amani kwenye eneo hilo la mashariki ya kati.

Tony Balir ameunga mkono hatua ya rais Mahmoud Abbas ya kuitisha uchaguzi wa mapema kwa ajili ya kumaliza mvutano kati ya serikali ya Hamas na chama cha Fatah juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Blair ambaye yuko mjini Tel Aviv Israel ametokea Iraq ambako alikuwa na mazungumzo na viongozi wa kisiasa na kukutana na baadhi ya wanajeshi wa Uingereza walioko nchini Iraq.