JERUSALEM.Katibu mkuu wa umoja wa mataifa aitaka Israel iondoshe hatua za kijeshi dhidi ya Lebanon
30 Agosti 2006Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan yupo nchini Israel kufuatia ziara yake nchini Lebanon ambako alishuhudia maafa yaliyosababishwa na vita kati ya majeshi ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah.
Bwana Annan anatazamiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Israel juu ya hatua za kijeshi zinazo tekelezwa na nchi hiyo dhidi ya Lebanon.
Katibu mkuu anaitaka Israel kusitisha hatua ya kuzifunga bandari na viwanja vya ndege nchini Lebanon.
Wakati huo huo takriban wanajeshi 1000 wa Italia wamo njiani kuelekea Lebanon ikiwa ni sehemu ya mchango wa nchi hiyo kwa ajili ya jeshi la kulinda amani kusini mwa Lebanon.
Italia inatarajiwa kuchukuwa hatua za kukiongoza kikosi cha kimataifa cha kulinda amani huko kusini mwa Lebanon kutoka kwa Ufaransa mwezi februari mwaka ujao.