1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:.Ehud Baraka kuongoza chama cha Labour

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs7

Waziri mkuu wa zamani nchini Israel Ehud Barak amechaguliwa kukiongoza chama cha Labour dhidi ya mpinzani wake mkuu wa zamani wa usalama Ami Ayalon.

Katika sherehe za ushindi wake Barak ametaka pawepo mshikamano wa chama na kuahidi kurejesha hadhi ya jeshi la Israel.Barack anatarajiwa kuchukua wadhifa wa waziri wa Ulinzi kutoka kwa Amir Peretz katika serikali ya waziri mkuu Ehud Olmert.

Kabla ya uchaguzi wa chama cha Labour bwana Barak alimtaka waziri mkuu Olmert kujiuzulu kufuatia kushindwa katika vita dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon. Aidha bwana Barak amegusia kwamba atakiondoa chama chake cha Labour katika muungano na chama cha Kadima cha waziri mkuu Olmert.