Jerusalem. Jeshi la Israel lapambana na majeshi ya Hizboullah huko Lebanon.
30 Juni 2005Jeshi la Israel imetangaza makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika ukanda wa Gaza kuwa ni eneo lililofungwa la kijeshi.
Hii inafuatia ghasia zilizotokea jana kati ya Wapalestina , majeshi ya usalama na walowezi wanaopinga mpango wa serikali yao wa kuondoka katika eneo la Gaza.
Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon hapo mapema aliamuru majeshi ya usalama kuchukua kila hatua inayowezekana kuzuwia waandamanaji kuchafua mpango wa kujiondoa kutoka Gaza.
Katika maeneo mbali mbali nchini Israel , waandamanaji walizuwia barabara kuu kwa kukaa chini barabarani, na kuzuwia magari kupita katika wakati watu wanarejea kutoka kazini.
Polisi wamewakamata zaidi ya waandamanaji 100.
Mpango wa Israel wa kujiondoa kutoka Gaza umepangwa kuanza katikati ya mwezi wa August.