JERUSALEM: Israel yajadili makubaliano ya Hamas na Fatah
11 Februari 2007Matangazo
Baraza la mawaziri la Israel limekutana kujadili suala linalohusika na serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Wapalestina.Kabla ya kikao hicho, waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert alisema, serikali ijayo ya Hamas na Fatah lazima itimize masharti ya kundi la kimataifa la pande nne. Miongoni mwa masharti hayo ni kutambua haki ya kuwepo taifa la Israel.Siku ya Alkhamisi mjini Mekka,makundi hasimu ya Kipalestina,chini ya usimamizi wa Saudia Arabia,yalikubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.Baadae chama cha Hamas kilisisitiza kuwa hakitoitambua Israel.