JERUSALEM : Israel yaachilia euro milioni 77 za Wapalestina
20 Januari 2007Israel imehamisha kwa kuzipeleka kwa Mamlaka ya Palestina euro milioni 77 fedha za michango ya Wapalestina ilizokuwa imezizuwiya.
Afisa wa serikali ya Israel amesema fedha hizo zitatumiwa kwa ajili ya dhamira za amani na pia kuimarisha kikosi cha ulinzi cha Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kama ilivyokubaliwa na pande zote mbili za Palestina na Isarel mwezi uliopita.
Fedha hizo ni sehemu ya takriban euro milioni 510 ya ushuru wa forodha ambao Israel iliukusanya kwa niaba ya Wapalestina.Israel ilisita kuzihamisha fedha hizo wakati kundi la Hamas lilipochukuwa madaraka ya serikali ya Mamlaka ya Palestina baada ya kushinda uchaguzi hapo mwezi wa Januari mwaka jana.
Israel,Marekani na Umoja wa Ulaya wanalihesabu kundi la Hamas kuwa la kigaidi.