1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel kuondoa makazi ya wayahudi Ukingo wa Magharibi

14 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXD

Israel imetangaza kwamba imeafikiana juu ya kuyaondoa makazi 24 ya walowezi wa kiyahudi yaliyojengwa kinyume cha sheria katika eneo la Ukingo wa Magharibi, tangu kuingia madarakani kwa waziri mkuu Ariel Sharon mwaka 2001.

Kuondolewa kwa makazi hayo ni mojawapo ya maagizo yaliyotolewa kwenye mpango wa amani wa Road map.Tangazo la Israel limekuja sawia na ziara ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan katika eneo hilo la Mashariki ya kati.

Annan amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon. Leo anatarajiwa kukutana na rais Mahmoud Abbas wa Palestina mjini Ramallah.

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Annan katika eneo hilo la Mashariki ya kati tangu miaka minne na amesema kuna matumaini ya kupatikana amani.