JERUSALEM: Ehud Olmert amehojiwa kuhusu vita vya Lebanon
1 Februari 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert ameanza kutoa ushahidi wake mbele ya tume maalum ya serikali, iliyoundwa kuchunguza vita vya mwaka jana kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon. Viongozi wa serikali na wakuu wa majeshi, walilaumiwa vikali jinsi walivyoendesha vita hivyo vya mwezi mmoja.Waziri mkuu Olmert ni wa mwisho kutoka jumla ya mashahidi 70 waliohojiwa mbele ya tume ya uchunguzi,inayotazamiwa kutoa ripoti yake ya kwanza kati kati ya mwezi wa Machi.