1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Annan ziarani Mashariki ya Kati

13 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXJ

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,bwana Kofi Annan hii leo anaanza ziara yake ya siku tatu katika Mashariki ya Kati kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa Waisraeli na Wapalestina.Hii leo Annan atakutana na waziri mkuu Ariel Sharon wa Israel kuzungumzia njia za kuchangamsha utaratibu wa amani.Siku ya jumatatu atakwenda Ramallah kwenye Ukingo wa Maghariibi kukutana na kiongozi wa Wapalestina Mahmud Abbas.Kofi Annan siku ya jumanne atakuwa pamoja na zaidi ya viongozi 30 wa madola na mawaziri mjini Jerusalem,kwa ufunguzi wa jumba jipya la makumbusho ya maangamizi-Yad Vashem.Hii ni ziara ya mwanzo kufanywa na Kofi Anna katika eneo hilo la Mashariki ya Kati tangu miaka minne na amesema kuna matumainio mema kuhusu utaratibu wa amani.