1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je,mpango wa kuufufua uchumi utafanya kazi ?

14 Januari 2009

Ndio mada kuu ya wahariri leo.

https://p.dw.com/p/GY99
Angela MerkelPicha: AP

Uchambuzi katika safu za wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani takriban umetuwama juu ya mada moja tu:Mapendekezo ya serikali ya Ujerumani jinsi ya kuutia jeki uchumi.Serikali ya Kanzela Angela Merkel, imeidhinisha kitita cha Euro bilioni 50 katika mradi wake wa pili wa kuufufua uchumi.

Gazeti la Emder Zeitung kuhusu mada hii,laandika:

Mpango wa pili wa kuustawisha uchumi sasa umepitishwa; na Kanzela Angela Merkel hakuachakujitapa kuuita mradi mkubwa kabisa katika historia ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerimani.Hatukatai kwamba fedha nyingi zitatumika,lakini nani zinamfaidia ?

Kwa ufupi,wengi watanufaika kidogo,lakini hakuna ataefaidika sana.Tumuangalie raia wa kawaida.Familia ya kawaida, mbali na ruzuklu inayotolewa kwa watoto wao,itaondokea kwa kadiri ya pato lao kati ya Euro 15 na 20. Familia kama hiyo itajikuta pekee imekabiliwa na mzigo mwishoni mwa mwaka wa kulipa deni la ziyada gesi iliotumia mwaka mzima linalofikia Euro mia kadhaa.Kwa njia hii ,familia hiyo kumudu kununua bidhaa ili kuutia jeki uchumi,haiyumkiniki."

Gazeti la Reutlinger General-Anzeiger linahisi katika kipindi hiki cha msukosuko mkubwa wa fedha tangu kupita miongo mingi,wanasiasa wenye madaraka wameonesha uwezo wao wa kutenda.gazeti laongeza:

"Uamuzi wa aina hiyo wa serikali, unasaidia kurejesha imani iliopotea.

Hatahivyo,nadra kuwa rahisi hivyo, kwa watawala kutumia mabilioni ya fedha kwa gharama ya kizazi kijacho cha walipa kodi.

Flensburger Tageblatt linauliza :Iwapo kwa kutunukiwa fedha zaidi wanunuzi kweli watautia jeki uchumi au wataziweka tu fedha zao upande,sio tu itategemea imani yao kwa siku zijazo.

Kuanza tangu sasa kuutoa maanani hautakua na athari yoyote mpamngo huo wa kuufufua uchumi,ni kupalilia hali ya kuvunja moyo.Kutofanya hivyo lakini, hakuna maana kupongeza maamuzi hayo yaliopitishwa na serikali ya muungano.

Nalo gazeti la Sąchsische Zeitung kutoka Dresden, linaona mradi huu wapili wa kuufufua uchumi una nafuu ya kufanya kazi tangu haraka hata katika muda mfupi ujao.

Katika kipindi kifupi, kitita cha Euro 100 kinachotolewa kwa kila mtoto

kingeonesha si sera barabara ya kiuchumi kufanya hivyo.Lakini kwa kuwa hatua hiyo inafuatiwa katika muda usio mrefu ujao na kupunguzwa kwa kodi ya mapato na matumizi katika ujenzi wa barabara mpya na kukarabati mashule,mpanguo huo utasaidia.

Mwishoe,gazeti la Neue Osnabrucker Zeitung linahisi ingawa zinatolewa fedha nyingi lakini athari zake si kubwa:

Ni kwa jicho hilo ndio uangalie mpango huo wa pili wa serikali ya Ujerumani wa kuutia jeki uchumi.Kwani, ingawa unatia shime katika kuustawisha uchumi kuanzia nusu ya pili ya mwaka huu,hatahivyo, haulingani kabisa kati ya matumizi na gharama zake.