1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JEDDAH:Saudi Arabia mbioni kufungua ubalozi wake Iraq

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbM

Saudi Arabia imesema leo kuwa itapeleka ujumbe nchini Iraq wiki ijayo katika maadalizi ya kuufungua ubalozi wake mjini Baghdad ikiwa ni zaidi ya miaka minne toka majeshi ya Marekani na washirika yalipoivamia Iraq.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Prince Saud al Faisal amesema kuwa hatua hiyo ni ishara ya nchi yake kurejesha uhusiano kamili na Iraq

Nchini Iraq kwenyewe Waziri Mkuu wa serikali ya kishia , Nour al Maliki amepata pigo lingine baada ya mawaziri wanne zaidi kutangaza kususia vikao vya baraza la mawaziri.

Wiki iliyopita kundi kubwa la mawaziri wa upande wa wasunni lilijiondoa serikali kutokana na waziri mkuu huyo kushindwa kutimiza matakwa yao yakiwemo ya kupewa usemi mkubwa katika masuala ya kiulinzi.

Wakati huo huo takriban watu 28 wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga katika mji wa Tal Afar uliyoko kaskazini mwa Iraq.

Kwengineko askari wanne wa Marekani wameuawa wakati waliposhambuliwa na bomu huko katika jimbo la Diyala.Duru za jeshi la Marekani zimesema kuwa askari wengine 12 wamejeruhiwa.