1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jean-Claude ataka kukomeshwa kwa ukaguzi wa mipaka katika EU

23 Novemba 2024

Rais wa zamani wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jean-ClaudeJuncker, ambaye pia alikuwa waziri mkuu wa Luxembourg amekosoa kuanzishwa tena kwa ukaguzi wa mipaka wa Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4nLm0
Jean-Claude Juncker  / Ukraine
Jean-Claude Juncker, Rais wa zamani wa Kamisheni ya Umoja wa UlayaPicha: Andreas Arnold/dpa/picture alliance

Kiongozi huyo wa zamani ameliambia shirika la utangazaji la hapa Ujerumani DPA kwamba yeyote anaefikiri anaweza kuwakamata wakimbizi na watu wengine kwa waranti ni kosa. Alisema kuwa wasafirishaji haramu wanafanya kila wawezalo kuepuka ukaguzi rasmi wa polisi. Na kuongezaa kwamba ukweli huo unajidhihirisha katika maeneo ya Luxembourg, ambao kuna kuwa na msongamano mkubwa juu ya mipaka ya Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji. Ujerumani ilirejesha hatua za ukaguzi wa  mipaka yake yote Septemba 16, kwa lengo la kudhibiti wimbi la wahamiaji na kulinda usalama wa ndani. Hatua ambayo pia inatekelezwa na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.