Bajuni ni moja ya makabila ya jamii ya waswahili wa mwambao wa Kenya na pengine ni moja ya jamii zisizofahamika sana nchini Kenya. Hii ni jamii inayotajwa kuwa na idadi ya watu wasiozidi laki moja,lakini yenye utajiri mkubwa wa tamaduni za kale za waswahili wa mwambao wa pwani ya Lamu huko Kenya. Makala ya Utamaduni na sanaa inaangazia shina la kabila la Bajuni, mila na desturi zao.