Kwa miongo kadhaa sasa baadhi ya nchi katika bara la Afrika zimekuwa zikikabiliwa na migogoro, mingi ya migogoro hiyo ikiwa ni ya kisiasa. Viongozi wa kisiasa walio na ulafi wa madaraka wameng'ang'ania mamlakani huku wakifuja raslimali na kuzitumbukiza nchi zao katika mizozo ya kiuchumi na kibinadamu.