Kwa mila za kiafrika, linapokuja suala la ndoa, huhitajika mshenga, ambaye yeye aghalabu wajibu wake ni kupeleka ujumbe kwenda upande wa mwanamke, kueleza lengo la kutaka kuoa binti wa familia ile. Mshenga Revocatus Buberwa amekuwa chanzo cha wapendanao wengi kufanikisha ndoa zao akiwa amekwisha waunganisha wanandoa zaidi ya 200. Florence Majani alizungumza nae.