Hatua ya Saudi Arabia kutangaza kwamba itapunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa takriban milioni moja kwa siku kuanzia mwezi Julai, imezua hofu ya kudorora zaidi kwa uchumi wa dunia ambao bado haujaimarika kufuatia janga la Uviko-19. Hatua hiyo iliyotangazwa na Saudi Arabia katika mkutano wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi zaidi duniani OPEC+ itakuwa na athari gani kwa mataifa ya Afrika?