Pande mbili zinazohasimiana nchini Sudan siku ya Alhamisi zilikubaliana kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa 72, ili kuruhusu huduma za kiutu kuendelea na kutoa nafasi kwa nchi za kigeni kuwaondoa raia wao, ingawa mapigano bado yamekuwa yakiendelea kwenye baadhi ya maeneo ya mji mkuu, Khartoum. DW imezungumza na mchambuzi Martin Oolo.