Kamala Haris amekubalia kugombea urais kupitia chama cha Democrat. Katika mkutano mkuu wa chama uliofanyika Chicago, Harris alisema hadithi na historia yake ya kuwa mwendesha mashtaka inamfanya kuwa na sifa za kipekee kulinda maslahi ya Wamarekani dhidi ya rais wa zamani Donald Trump ambaye alidai anatanguliza maslahi binafsi. Hotuba hii ilidadavuliwa na mchambuzi wa siasa Prof David Monda.