Je, Dlamini-Zuma ataweza kuiongoza Afrika kusimama imara?
23 Julai 2012Matangazo
Suali linaoulizwa na wengi ni ikiwa kuchaguliwa huku kwa mwanamke kuliongoza bara la Afrika kuna maana yoyote ile katika mabadiliko ya taswira ya uongozi kwenye vichwa vya Waafrika, wanaoaminika kumpa nafasi zaidi mwanamme katika utawala? Je, Afrika inaongoza njia kwa masuala ya usawa wa kijinsia? Na kubwa kuliko yote, je Dlamini-Zuma atafanya kipi kipya ambacho mtangulizi wake, Jean Ping wa Gambia, kilimshinda?
Othman Miraji anaongoza mjadala mbele ya kipindi cha Maoni kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW. Kusikiliza mjalada huo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikinioni hapo chini.
Mwendeshaji: Othman Miraji
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman