Jarida la Ufaransa lililofungiwa Burkina Fasso lashutumu
27 Septemba 2023Katika taarifa yake iliyotolewa usiku wa kuamkia leo, jarida hilo la Jeune Afrique limelaani kile imekitaja kuwa "shambulizi dhidi ya uhuru wa habari" kwenye taifa lililoshuhudia mauaji ya mwandishi mashuhuri wa habari za uchunguzi Norbert Zongo mnamo mwaka 1998.
Limesemamarufuku ya utawala wa jeshini hatua nyingine ya kuifanya kanda ya Sahel na nchi ya Burkina Fasso kuwa eneo ambalo halipati taarifa chini ya misingi inayokubalika.
Soma pia:Wenye itikadi kali wauwa 33 Burkina Fasso
Uamuzi wa kulipiga marufuku jarida hilo ulitolewa siku ya Jumatatu baada ya manajerali kulituhumu Jeune Afrique kuchapisha makala mbili zenye lengo la kulipaka matope jeshi na kuleta mtafaruku nchini humo.
Tangu jeshi lilipochukua madaraka kwa nguvu mwaka 2022, vituo kadhaa vya habari ikiwemo televisheni na redio vimefungwa na waandishi habari wa kimataifa wametimuliwa, hususani wale wa kutoka Ufaransa.