Japan yasitisha utiririshaji wa maji ya Fukushima
15 Machi 2024Matangazo
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.8 katika kipimo cha Richta, limepiga pwani ya mkoa wa kaskazini mashariki wa Fukushima ambako ndiko kunapatikana kinu hicho cha nyuklia.
Kampuni ya umeme ya Tokyo TEPCO imesema mapema leo kwamba wameamua kusitisha kwa muda shughuli katika kinu hicho kwa sababu za kiusalama. Saa chache baadae kampuni hiyo ilisema hakuna kasoro yoyote iliyogunduliwa na hakuna uvujaji wa mionzi.
Agosti mwaka uliopita, kampuni ya TEPCO ilianza kutiririsha maji taka kwenye Bahari ya Pasifiki ambayo yalikuwa yamekusanywa kutoka kinu cha Fukushima Daiichi kilichoharibiwa na mkasa wa Tsunami wa 2011. Ajali hiyo ilikuwa mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya nyuklia duniani.