Japan yashukisha kiwango cha tahadhari kuhusu tsunami
1 Januari 2024Tetemeko hilo kubwa la 7.6 kwenye kipimo cha Richter lilisababisha kuzuka kwa moto na kuporomoka kwa majengo katika maeneo ya Magharibi ya kisiwa chake kikubwa cha Honshu.
Haikubainika wazi idadi ya watu waliofariki ama kujeruhiwa.
Msemaji wa serikali Yoshimasa Hayashi, amesema takriban nyumba sita ziliharibiwa na matetemeko hayo huku watu kadhaa wakikwama ndani yake.
Soma pia:Tsunami yaipiga Japan
Moto pia ulizuka katika mji wa Wajima na takriban nyumba 30,000 kukosa huduma za umeme.
Awali Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa tahadhari ya tetemeko kubwa la chini ya bahari katika eneo la Ishikawa na onyo lamatetemeko ya wastani kwa maeneo mengine ya Pwani ya Magharibi ya kisiwa cha Honchu pamoja na visiwa vya Hokkaido katika eneo la Kaskazini.
Masaa machache baadaye, Mamlaka hiyo ilishusha kiwango cha tahadhari hii ikimaanisha kuwa mawimbi huenda yakafikia hadi mita 3.