1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Japan yalalamika baada ya meli za China kutumia bahari yake

7 Juni 2024

Japan imewasilisha malalamiko malalamiko Beijing, baada ya meli nne za China zinazoaminika kubeba silaha kuonekana katika eneo la visiwa linalozozaniwa katika bahari ya mashariki mwa China, ambalo linadhibitiwa na Japan.

https://p.dw.com/p/4gngj
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida
Waziri Mkuu wa Japan Fumio KishidaPicha: Noriaki Sasaki/The Yomiuri Shimbu/AP/picture alliance

Msemaji mwandamizi wa serikali ya Japan, Yoshimasa Hayashi amewaambia waandishi habari kwamba ni mara ya kwanza meli nne za China zinazobeba silaha kuingia kwenye eneo hilo la bahari la Japan, linalozunguka visiwa vya Senkaku.

Meli hizo ziliondoka baada ya muda wa  saa mbili kufuatia onyo lililotolewa na walinzi wa pwani wa Japan.

Soma pia:Viongozi wa Korea Kusini, China, Japan wakutana Seoul

China pia inadai eneo hilo inaloliita Diaoyus ni milki yake na limekuwa pia kwa muda mrefu likizusha mvutano mkali baina ya majirani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW