Japan yaiwekea vikwazo Korea ya kaskazini
19 Septemba 2006Matangazo
Japan imechukuwa vikwazo vingine vya kiuchumi dhidi ya Korea ya kaskazini kufuatia jaribio la kurusha kombora lililofanywa na nchi hiyo mnamo mwezi Julai mwaka huu. Vikwazo hivyo vinawapiga marufuku wa kutoa pesa kutoka Benki au kuzichukuwa kuzirudisha nyumbani kwa watu au makundi ya watu wanaokuwa na uhusiano kwa njia moja ama nyingine na mpango wa kijeshi wa Korea ya kaskazini. Nchi nyingine ambayo imeyichukulia vikwazo Korea ya kaskazini ni Australia. Vikwazo hivyo ni vya kifedha dhidi ya makampuni na mtu mmoja anayeshukiwa kuisaidia Korea ya kaskazini katika kugharamia mpango wake wa kutengeneza silaha za kinyuklia.