Japan na China zafanya mazumngumzo
28 Desemba 2007BEIJING:
Mazungumzo ya viongozi wa China na Japan yanaendelea vizuri.
Hii ni kwa mujibu wa viongozi wa nchi hizo mbili.Waziri Mkuu wa Japan-Yasuo Fukuda aliwasili alhamisi China kwa ziara rasmi ya siku nne ambapo atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Wen Jia-Bao.
Miongoni mwa masuala yakujadiliwa ni pamoja na mpango wa nuklia wa Korea kaskazini na vilevile kuhusu kubadilika kwa hali ya hewa na mvutano wa kimpaka hususan kuhusu visima vya gesi katika eneo la bahari ya mashariki ya China.Japan imeihimiza China kutumia umaarufu wake kuleta mageuzi katika masuala nyeti ya dunia kama vile suala la kubadilika kwa hali ya hewa.
Waziri mkuu wa China amsema kuwa uhusiano kati ya China na Japan umeimarika.
Nchi hizo mbili zimekuwa na uhasama unaoanzia wakati wa vita vya miaka mingi ,mali na mipaka.Waziri mkuu wa japana pia amepangiwa kukutana na rais wa China -Hu Jintao.