1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaKorea Kusini

Japan kuanza kutiririsha maji ya kinu cha Fukushima

24 Agosti 2023

Japan hii leo itaanza kutitirisha baharini maji yaliyosafishwa na kuondolewa viambata vya mionzi kutoka kinu cha nyuklia cha Fukishima ambacho kiliharibiwa na janga la Tsunami la mnamo mwaka 2011.

https://p.dw.com/p/4VWFm
Waandamanaji wa Korea Kusini
Mpango wa kutiririsha maji hayo umezusha ukosoaji kutoka China, Korea Kusini na Korea Kaskazini Picha: Jung Yeon-je/AFP

Kampuni inayosimamia kinu hicho ya Tepco, imesema maji hayo yatatitirishwa kwa awamu kuingia kwenye bahari ya Pasifiki na kiwango cha kwanza kitakuwa lita za ujazo 7,800 na itachukua muda wa siku 17 kukamilika.

Uamuzi wa kuyafungulia maji hayo kuingia baharini umezusha ukosoaji mkali kutoka China ambayo imejibu kwa kupiga marufuku uingizaji wa vyakula vya baharini kutoka miji ya Japan iliyo karibu na eneo la bahari ambalo maji hayo yataingia.

Wasiwasi uliopo ni kuwa akiba hiyo ya maji iliyotumika kupooza mitambo ya nyuklia ya Fukishima huenda bado ina kiwango kikubwa cha mionzi ya sumu.Japan yenyewe imesisitiza zoezi hilo ni salama na mnamo mwezi Julai, Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, lilitoa ithibati ya maji hayo kutitirishwa baharini likisema yamekidhi viwango vya kimataifa vya usalama.