Jamhuri ya Afrika ya Ufaransa yaikaripia Ufaransa
20 Oktoba 2021Hayo yanajiri kufuatia mvutano unaoendelea kuhusu uwepo wa wapiganaji wa Kirusi kwenye taifa hilo linaloandamwa na machafuko.
Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Sylvie Mbaipo-Temon amesema tabia ya Ufaransa ya kutaka kutawala maamuzi ya serikali mjini Bangui ni sharti ikomeshwe ikiwemo shinikizo lake la kupinga uwepo wa mamluki kutoka Urusi nchini humo.
Tamko hilo linafuatia madai yaliyotolewa na mwezake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian aliyesema mamluki wa Urusi waliopelekwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kutuliza uasi ndiyo wanazidisha machafuko ikiwemo matendo ya kikatili.
Urusi ilipeleka washauri wa kijeshi nchini humo tangu mwaka 2018 na baadae kutuma kundi la wapiganaji wa kampuni binafsi ya Wagner kuisaidia serikali hatua ambayo imeikasirisha Ufaransa, ambayo ni mkoloni wa zamani.