1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Afrika ya Kati

Jamhuri ya Afrika ya Kati yakumbwa na ongezeko la uasi

18 Juni 2024

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kuongezeka kwa shughuli za makundi yaliyojihami kwa silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

https://p.dw.com/p/4hBfw
Jamhuri ya Afrika ya Kati yakabiliwa na ongezeko la shughuli za waasi, Umoja wa Mataifa wasema.
Jamhuri ya Afrika ya Kati yakabiliwa na ongezeko la shughuli za waasi, Umoja wa Mataifa wasema.Picha: Barbara Debout/AFP

Umoja huo umesema makundi hayo yanatatiza mazingira ya usalama na kusababisha kusambaa kwa mzozo hadi katika nchi jirani Sudan.

Jopo la wataalamu katika ripoti yake mpya limetaja visa vilivyothibitishwa vya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Sudan katika eneo la mpaka na vya wapiganaji wa RSF wanaovuka na kuingia nchini humo kujifunza kutoka kwa makundi yenye silaha ya Afrika ya Kati.

Sudan ilitumbukia kwenye vita katikati ya mwezi Aprili mwaka uliopita kufuatia mvutano kati ya majenerali wa jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF.

Mapigano yalisambaa kwenye maeneo mengine ambayo ni pamoja na Darfur, inayopakana na mkoa wa Vakaga ulioko kaskazinimashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.