1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

James Rodriguez aanza tena kufanya mazoezi

12 Desemba 2014

James Rodriguez wa Real Madrid ameanza kukimbia tena baada ya kupata maumivu katika paja na anaweza kushiriki katika michezo ya kombe la dunia la vilabu itakayofanyika wiki ijayo nchini Morocco.

https://p.dw.com/p/1E3Pm
James Rodriguez Real Madrid Spieler
Picha: picture alliance/AP Photo

Mshambuliaji huyo kutoka Colombia alijeruhiwa katika ushindi wa mabao 3-0 mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Celta Vigo katika La Liga na hakuweza kucheza katika mchezo dhidi ya Almeria jana Ijumaa, wakati mabingwa hao watetezi wa bingwa wa Ulaya wakiwania kupata ushindi wake wa 20 katika la Liga mfululizo.

Kocha Carlo Ancelotti ameeleza kuwa mchezaji huyo pia hataweza kucheza katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia, dhidi ya ama Cruz Azul ya Mexico ama Western Sydney Wanderrers ya Australia Jumanne ijayo, lakini amesema anaweza kucheza katika fainali, iwapo Madrid watafanikiwa kufika huko.

Atletico Madrid imepiga marufuku bendera zenye uhusiano na kundi la mashabiki sugu la Frente Atletico katika uwanja wao baada ya shabiki wa klabu ya Deportivo La Coruna kuuwawa kabla ya mchezo wao katika uwanja wao.

Nae kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameanza majadiliano ya mkataba wake na shirikisho la kandanda la Ufaransa ili kuweza kupakia kwa muda mrefu katika wadhifa huo ambapo rais wa shirikisho hilo anataka Deschamps abakie hapa baada ya fainali za Euro 2016 zitakazofanyika nchini humo.

Kocha huyo wa zamani wa Monaco na Juventus ambaye ameiongoza Ufaransa kunyakua taji la kombe la dunia mwaka 1998 na Euro 2000 akiwa nahodha , amekataa kufichua ishara zozote lini mkataba wake utarefushwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman