1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA:Indonesia yamuunga mkono Rais Mugabe

7 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlN
Indonesia imesema leo hii kutokana na kuwa na ozoefu mmoja wa ukoloni wa kale na Zimbabwe ingeliweza kuelewa mpango tata wa nchi hiyo wa kunyakuwa mashamba ya wazungu na kuyagawa kwa wazalendo. Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia Hassan Wirajuda ametowa kauli hiyo baada ya kuhudhuria mkutano kati ya Rais Megawati Sukranoputri na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye yuko katika ziara isio rasmi nchini Indonesia. Mugabe ametaifisha zaidi ya mashamba 5,000 yaliokuwa yakimilikiwa na wazungu kwa ajili ya kuyagawa upya kwa wazalendo mafukara tokea mwaka 2000 na kuzusha shutuma za kimataifa.Kiongozi huyo pia yuko katika shinikizo la kimataifa kwa madai ya kukiuka haki za binadaamu na kuvuruga uchaguzi.