Jaji Nigeria awapa dhamana watu 10 walioshtakiwa kwa uhaini
11 Septemba 2024Jaji mmoja katika mahakama ya Nigeria, amewaachilia kwa dhamana watu 10 waliokuwa wameshtakiwa kwa kosa la uhainina kula njama ya kuchochea uasi wa kijeshi kufuatia maandamano yaliyozuka mwezi uliopita nchini humo, ya kupinga ongezeko la gharama za maisha.Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya
Jaji Emeka Nwite amewapa dhamana wanaume tisa na mwanamke mmoja kwa kutumia mamlaka yake baada ya kujiridhisha kutokana na tahmini aliyoifanya. Watuhumiwa hao wote walikanusha mashtaka yanayowakabili. Wanigeria waliandamana kwa siku 10 mwezi uliopita kulalamikia mfumuko wa bei uliosababisha hali ngumu ya maisha kwa wakaazi wengi. Maandamano hao yalishuhudia maelfu ya watu wakiingia mitaani, lakini yalidhibitiwa na vikosi vya usalama vilivyotawanywa katika miji ya nchi hiyo na takriban watu 13 waliuwawa.