SiasaItaly
Italia kufanya ibada ya kumuaga Silvio Berlusconi
14 Juni 2023Matangazo
Hafla hiyo ya kumuaga Berlusconi, aliyefariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 86, itafanyika katika kanisa kongwe la Duomo mjini humo na kuonyeshwa moja kwa moja kwenye skrini kubwa za uwanja huo.
Berlusconi, aliugua kwa miaka kadhaa, ijapokuwa alibakia kuwa kiongozi rasmi wa chama chake cha siasa za mrengo wa kulia cha Forza Italia, ambacho ni mshirika wa serikali ya muungano ya Waziri Mkuu Giorgia Meloni.
Soma pia: Waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi afariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.
Rais wa Italia Sergio Mattarella, Waziri Mkuu Meloni na Matteo Salvini, kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha League, ambacho ni sehemu ya serikali ya muungano, wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.