Israel yawauwa Wapalestina sita Ukingo wa Magharibi
8 Desemba 2023Hayo yameelezwa na wizara ya afya ya Palestina iliyosema Wapalestina hao walipigwa risasi na kuuwawa kwenye kambi ya Al-Fara inayopatikana karibu na mji wa Tubas.
Jeshi la Israel halijazungumza chochote kuhusu mauaji hayo. Wakati huo huo Israel imekubali kufungua mpaka wa Kerem Shalom kwa ajili ya kukagua misaada ya kibinaadamu inayopelekwa Gaza kupitia eneo la kivuko la Rafah.
Soma zaidi: Marekani imetilia shaka juhudi zinazofanywa na Israel za kuwalinda raia
Maafisa wa Marekani wamekuwa wakijadiliana kuhusu uwezekano wa kufunguliwa kwa mpaka huo kwa wiki kadhaa, ili kuharakisha mchakato wa ukaguzi wa malori ya misaada.
Aidha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili vita vya Gaza. Umoja wa Falme za Kiarabu uliwasilisha rasimu mpya ya azimio kutaka kusitishwa kwa mapigano Gaza.