ISRAEL YATIA KASI HUJUMA LEBANON
6 Agosti 2006Matangazo
TAARIFA YA HABARI 17.00 06-08-06
TYRE:LEBANON:
Israel leo iliendelea kutia kasi hujuma zake za mabomu katika vituo kadhaa vya wapiganaji wa Hizbollah na kumuua mwanamgambo wa Palestina huku jeshi lao likijaribu kusonga mbele kusini mwa Lebanon.Hujuma hizi katika siku ya 26 imesababisha kuuwawa kwa raia 9 na mfuasi wa kipalestina anaelemea Syria pamoja na kuwajeruhi raia wengine 10 kwa muujibu wa polsi ya Lebanon.Hivi punde mashambulio makali ya mabomu yamefanywa mjini na Israel katika kitongoji cha kusini cha mji mkuu Beirut.