1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaondoa pia viuizi vya baharini dhidi ya Lebanon.

Mohammed Abdulrahman8 Septemba 2006

Harakati za kibalozi mashariki ya kati zaimarika, akiwemo Waziri wa nje wa Ujerumani Steinmeir.

https://p.dw.com/p/CHLM
Wazri wa nje Steinmeier akiwa na maafisa wa Polisi wa Ujerumani mjini Beirut.
Wazri wa nje Steinmeier akiwa na maafisa wa Polisi wa Ujerumani mjini Beirut.Picha: AP

Israel leo imeondoa hatua yake ya vizuizi vya baharinii vya miezi miwili dhidi ya Lebanon,baada ya manuwari za nchi za Ulaya kuanza kupiga doria katika fukwe na mwambao wa Lebanon, kuzuwia uingizaji silaha kwa wapiganaji wa Hezbollah. Wakati huo huo harakati za kibalozi kutoka pembe mbali mbali za dunia zimeimarishwa katika jitihada za kuupa nguvu usimamishaji mapigano na kuyafufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati.Miongoni mwa wajumbe walioko katika eneo hilo ni Waziri wa kigeni wa Ujerumani Frank Walter-Steinmeir .

Kiongozi wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa mataifa mfaransa Meja Jenerali Alain Pellegrini alisema amearifiwa na maafisa wa Israel juu ya kumalizwa hatua hiyo ya kulizingira eneo la bahari la Lebanon , na pia na kamanda wa kikosi cha majini cha Italia ambaye anakiongoza kikosi cha kimataifa.

Tukio hilo linafuatia pia kumalizwa vizuizi vya anga na usafiri wa anga kuingia Lebanon hapo jana.

Wakati huo huo, jitihada aza kibalozi za kimataifa zinaendelea kupata kasi, ili kuimarisha usimamishaji mapigano na kuyafufua mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati. Mawaziri kadhaa wa mambo ya nchi za nje wamo ziarani katika eneo hilo, akiwemo Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ambaye alikua na mazungumzo leo na Waziri wa ulinzi wa Israel Amir Peretz.

Mjini Tel Aviv Bw Peretz alimueleza Wazieri Steinmeier kwamba Israel iknatarajia kukamilisha kuondoka Lebanon katika muda wa majuma mawili, mara shughuli za uratibu pamoja na jeshi la umoja wa mataifa zitakapomalizika. Pia alisema Ujerumani inaweza kutoa mchango muhimu katika juhudi za kuachiwa huru wanajeshi wawili wa Israel waliotekwa nyara Julai 12 na Hizbollah.

Waziri Steinmeeir aliwasili Israel akitokea Lebanon , ambako baada ya mazungumzo na Waziri mkuu Fuoad Siniora, aliwaambia waandishi habari kwamba Bw Siniora ametuma barua kwa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, kuomba Ujerumani ishiriki katika jeshi la umoja huo nchini Lebanon. Bw Steinmer alifuatana na baadhi ya maafisa wa kikosi cha ulinzi wa mpakani na wa ushuru, ambao wako Lebanon wakiwa washauri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini humo.

Kwa hivi sasa kushiriki kwa Ujerumani katika jeshi la umoja wa mataifa kumezuiwa kutokana na mkutano juu ya wakati wsa kutumwa na jinsi watakavyohusika. Huenda kikosi cha majini kikatumwa katika kipindi cha majuma mawili au matatu yajayo.

Mawaziri wengine wa kigeni walioko katika eneo hilo kuimarisha jitihada za kibalozi ni Waziri wa kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na Italia Massimo DÁlema ambaye nchi yake inakiongoza kikosi cha kimataifa nchini Lebanon.