Israel yafanya mashambulizi zaidi Gaza
17 Mei 2021Matangazo
Miripuko mikubwa imeutikisa mji huo kutoka kusini hadi kaskazini kwa dakika 10 mfululizo, ikiwa ni mashambulizi makubwa zaidi kuliko yaliyowahi kufanywa kwa muda wa saa 24 zilizopita.
Jumla ya Wapalestina 42 wameuawa kwenye mashambulizi hayo ya hivi karibuni zaidi kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ambao wanatawala Gaza.
Jeshi la Israel limesema limeshambulia nyumba za makamanda wa Hamas katika maeneo mbalimbali ya Gaza.