1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yauzingira mji wa Gaza huku idadi ya vifo ikiongezeka

8 Novemba 2023

Licha ya miito yakusitisha mapigano, jeshi la Israel limeendeleza mashambulizi huko Gaza katika dhamira yake ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4YYOQ
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Picha: imago images/Xinhua

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema mji wa Gaza umezingirwa huku waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant akisema kwa sasa wameingia katikati mwa jiji hilo. 

Akiwa mjini Ramallah, Waziri ya afya  wa Palestina Mai al-Kaila amesema hadi sasa, kunazaidi ya watu 10,400 waliouawakutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza na zaidi ya wengine 25,000 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.

Ameongeza kuwa idadi hiyo haiakisi hali halisi kwani idadi kubwa ya watu bado wamefukiwa chini ya vifusi. Zaidi ya asilimia 70 ya waliouawa ni watoto, wanawake na wazee. Alisema

Soma pia:Jeshi la Israel limesema vikosi vyake sasa vinaendesha shughuli zake mjini Gaza.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema wastani wa watoto 160 wanauawa kila siku huko Gaza.

Israel inaishutumu Hamas kwa kujenga mahandaki ya kijeshi chini ya majengo ya hospitali, shule na misikiti, madai yanayokanushwa na kundi hilo la wanamgambo.