1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaamini Iran yataka kutengeneza silaha ya nyuklia

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CX5J

Serikali ya Israel inaamini kuwa Iran ina njama ya kutengeneza silaha za nyuklia,licha ya ripoti ya wapelelezi wa Marekani kusema kinyume na hayo.Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak amesema,baada ya Iran kusitisha mradi wake wa nyuklia,huenda kwa sasa inaendelea na mradi huo.Idara 16 za upelelezi za Marekani katika ripoti yao ya pamoja zimesema haidhihiriki kuwa Tehran inatengeneza silaha ya nyuklia,kama serikali ya Rais Bush ilivyokuwa ikidai tangu miaka miwili iliyopita.Kwa upande mwingine China imetoa mwito wa kuanzisha upya majadiliano pamoja na Iran.