SiasaBahrain
Israel, nchi za kiarabu wajadili usalama Abu Dhabi
11 Januari 2023Matangazo
Wajumbe kutoka Bahrain, Misri, Israel, Morocco, Umoja wa Falme za Kiarabu na Marekani walijadiliana njia za kuimarisha ushrikiano wa usalama kupitia ubadilishanaji wa taarifa kama sehemu ya kile kinachoitwa Kongamano la Negev, mkutano ulioanza baada ya kusainiwa mikataba ya kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi za Kiarabu na Israel.
Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Derek Chollet ameyaeleza mazungumzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Jumatatu Abu Dhabi kuwa mkutano mkubwa kati ya Israel na washirika wake wa Mashariki ya Kati, tangu kongamano la amani la Madrid mnamo mwaka 1991.