1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Ujerumani kusaini mkataba wa kununua silaha

28 Septemba 2023

Ujerumani na Israel zinatarajiwa Alhamisi kutia saini makubaliano ya kuiuzia Ujerumani mfumo wa ulinzi wa makombora aina ya Arrow 3.

https://p.dw.com/p/4WuMk
Mawaziri wa  mambo ya nje wa Israel na Ujerumani
Mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na Ujerumani Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Tukio hilo litakalotekelezwa na waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant na mwenzake wa Ujerumani Boris Pistorius litafanyika mjini Berlin Ujerumani.

Mfumo wa ulinzi wa Arrow 3 unakusudiwa kuipa Ujerumani na majirani zake ulinzi bora dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya makombora.

Makombora yanayoelekezwa na mfumo huo hulenga kudungua makombora ya masafa marefu ya adui yakiwa juu angani na kuyaharibu moja kwa moja.

Israel imesema mauzo hayo yatakayogharimu takriban dola bilioni 4.2 ndiyo mauzo makubwa zaidi ya silaha za kivita katika historia ya Israel.