1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na mpango wake wa kujenga makaazi zaidi mashariki mwa Jerusalem

23 Machi 2010

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema mpango wa serikali ya Israel wa kujenga makaazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem utayahujumu mazungumzo na wapalestina.

https://p.dw.com/p/MZwM
Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Lakini waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa nchi yake ina haki ya kujenga katika mji huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema hali iliyopo sasa kati ya Israel na Wapalestina haiwezi kudumishwa katika upande wowote kwa sababu hali hiyo inatishia kusababisha umwagikaji damu zaidi na kuzuia shabaha zinazolengwa.Akizungumza mjini Washington kwenye mkutano wa jumuiya inayoyapigia debe maslahi ya Israel nchini Marekani bibi Clinton aliiambia Israel kuwa ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi mashariki mwa mji wa Jerusalem unaihujumu hadhi ya Marekani kama msuluhishi wa kuaminika anaepaswa kuwa tayari kupongeza, na ikibidi kulaani vitendo vya kila upande katika mashariki ya kati.

Waziri Clinton aliwaambia wajumbe kwenye mkutano huo kwamba Marekani illipaswa kulaani ujenzi wa makaazi mapya mashariki mwa Jerusalem na kwenye Ukingo wa Magharibi ili kulinda uaminifu wake na kuhakikisha mazungumzo baina ya Israel na wapalestina yanasonga mbele. Lakini amewaambia waisraeli na wapalestina kuwa hali iliypo sasa haiwezi kudumishwa.Amesema hali hiyo inatishia kusababisha umwagikaji wa damu na hadaa ya malengo yasiyoweza kufikiwa. Hata hivyo waziri Clinton amesema ipo njia nyingine.

Flash-Galerie Hillary Clinton
Waziri wa mambo ya nje Bibi Hillary Clinton asema hali ya Israel na Palestina inatishia umwagikaji wa damuPicha: picture alliance / abaca

Lakini ipo njia nyingine inayoongoza kwenye amani na neema, kwa Israel, wapalestina na watu wote wa eneo la mashariki ya kati.

Hata hivyo pande zote ikiwa pamoja na Israel zinapaswa kufanya maamuzi magumu lakini ni ya lazima.

Lakini akizungmza kwenye mkutano wa kila mwaka wa jumuiya inayoyapigia debe maslahi ya Israel nchini Marekani, AIPAC, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema kuwa Jerusalem siyo sehemu ya kulowea bali ni mji mju mkuu wa Israel.Netanyahu ameeleza kuwa wayahudi walikuwa tayari wanaujenga mji huo miaka alfu 3 iliyopita na kwamba wanaendelea kuujenga leo. Waziri mkuu huyo ameeleza kuwa anafuata sera za serikali zote za Israel tokea mwaka 1967 baada ya Israel kushinda vita dhidi ya jirani zake wa kiarabu na kuiteka sehemu ya mashariki y a mji wa Jerusalem.

Ujenzi wa makaazi zaidi mashariki mwa Jerusalem na kwenye Ukingo wa Magharibi unaivuruga hali ya kuaminiana na unayatia mashakani mazungumzo-japo siyo ya ana kwa ana.

Bibi Clinton amesema mazungumzo hayo ndiyo msingi wa kuelekea kwenye mazungumzo kamili ambayo kila upande unayataka. Clinton amesema ujenzi wa makaazi mapya pia unahujumu fursa pekee ya Marekani ya kutoa mchango muhimu katika juhudi za kuleta amani.

Mwandishi/Mtullya Abdu /AFPE

Mhariri/ Saumu Mwasimba