1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Israel na Marekani kufanya mazungumzo juu ya uvamizi Rafah

Hawa Bihoga
1 Aprili 2024

Israel na Marekani zinafanya mazungumzo kuhusu mpango wa uvamizi wa ardhini wa vikosi vya Israel kwenye mji wa Rafah.

https://p.dw.com/p/4eJu8
USA Israel Joe Biden Benjamin Netanjahu
Picha: Avi Ohayon/Israel Gpo/Zumapress/imago images

Mazungumzo hayo yatafanyika kwa njia ya mtandao wiki moja baada ya Israel kuifutilia mbali safari iliyokuwa imepangwa ya kutuma ujumbe wake mjini Washington.

Mivutano kati ya washirika hao wawili imeongezeka kutokana na idadi kubwa ya vifo vya raia vinavyoshuhudiwa Ukanda wa Gaza na mashaka yamekuwa makubwa zaidi mjini Washington juu ya dhamira ya Israel ya kutaka kufanya operesheni ya kijeshi kwenye mji uliofurika watu wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Soma pia: Mashambulizi yaendelea Gaza huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza tena Cairo

Israel iliifuta ziara mjini Washington baada ya Marekani kutotumia kura yake ya turufu kuzuia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotoa mwito wa kusitishwa vita vya Gaza. Marekani ilijizuia kulipigia kura azimio hilo.

Katika hatua nyingine wakosoaji wa sera za serikali ya Israel wamepiga kambi kwenye mahema mbele ya majengo ya bunge mjini Jerusalem, ikiwa ni sehemu ya maandamano yaliyoingia siku ya nne.

Waandamanaji hao wanashinikiza serikali ijiuzulu, kuitishwa kwa uchaguzi mpya na kuwaachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas.