Makubaliano ya kusitisha mapigano Lebanon yakiukwa
28 Novemba 2024Jeshi la Israel limesema makubaliano hayo, yaliyosimamiwa na Marekani na Ufaransa, yalikiukwa baada ya kile ilichoita washukiwa, wengine wakiwa kwenye magari, kuwasili katika maeneo kadhaa ya ukanda wa kusini. Mbunge wa Hezbollah Hassan Fadlallah aliituhumu Israel kwa kukiuka mpango huo. Amewaambia waandishi habari kuwa Israel inaendelea kuwashambulia wanaorejea kwenye vijiji vya mpakani.
Kifaru cha Israel kiliyapiga leo asubuhi maeneo sita ya ukanda huo mpakani. Maeneo hayo yote yako umbali wa kilomita mbili tu kutoka mpaka wa Lebanon na Israel.
Israel yaendelea kuishambulia Hezbollah licha ya mpango wa usitishwaji mapigano
Jeshi la Israel limetangaza amri ya kutotembea nje usiku kusini mwa Lebanon kuanzia leo (28.11.2024)
Wakati huo huo, Wapalestina karibu 17 wameuawa kwenye mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza. Hayo yameripotiwa na madaktari wakati vikosi vya Israel vikiendeleza mashambulizi kwenye maeneo ya kati na kuvisogeza vifaru vyao ndani kabisa kaskazini na kusini mwa ukanda huo.