1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yakubali kusitisha mapigano kwa masaa manne kila siku

10 Novemba 2023

Ikulu ya White House imearifu kwamba Israel imekubali kuanza kusimamisha mapigano kwa masaa manne kila siku ili kuruhusu watu kuondoka kwenye eneo lenye mapigano.

https://p.dw.com/p/4Ye0u
Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama nchini Marekani John Kirby amesema Israel imekubali kusimamisha mapigano kwa masaa manne kila siku
Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama nchini Marekani John Kirby amesema Israel imekubali kusimamisha mapigano kwa masaa manne kila sikuPicha: Anna Moneymaker/Getty Images

Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama nchini Marekani John Kirby amesema Israel ingetangaza awamu ya kwanza ya kusimamisha mapigano na kuahidi kuwa itakuwa inatoa tangazo hilo masaa matatu kabla ya kuanza utekelezaji.

Kirby amesema hatua hiyo itaruhusu watu kuondoka, misaada ya kiutu kuingizwa Ukanda wa Gaza na pengine kutumika kama njia ya kuwapata mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Katika hatua nyingine, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amezungumza na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwa njia ya simu na kwa mara nyingine alisema Ujerumani inahimiza raia kulindwa na kusimamishwa mapigano ili kuruhusu misaada ya kiutu.