1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yamuidhinisha waziri mpya wa mambo ya nje

31 Desemba 2023

Serikali ya Israel imeidhinisha uteuzi wa Waziri mpya wa Mambo ya Nje Israel Katz, akichukua nafasi ya Eli Cohen.

https://p.dw.com/p/4akPs
Israel Jerusalem | Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Israel, Yisrael Katz
Yisrael Katz aliyekuwa Waziri wa masuala ya usafirishaji nchini Israel sasa amekuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni, katika mchakato wa kubadilishana nafasi hiyo kama ilivyokubalika hapo kabla.Picha: Sebastian Scheiner/AFP/Getty Images

Eli Cohen sasa atachukua nafasi ya Katz aliyekuwa waziri wa Nishati, ingawa ataendelea kuhudumu kwenye baraza la mawaziri la masuala ya usalama.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikubali mwaka uliopita kubadilisha mawaziri kwenye wizara hiyo ya mambo ya nje.

Mapema leo, Baraza la mawaziri aidha liliidhinisha kuahirishwa uchaguzi wa manispaa uliopangwa kufanyika mwezi Februari, hatua ambayo hata hivyo inasubiri kuidhinishwa na bunge.

Haya yanafanyika wakati Netanyahu akisema kwa mara nyingine kwamba vita vya Israel dhidi ya Hamas vitachukua muda mrefu na kwamba hadi sasa vikosi vya nchi hiyo vimewaua magaidi 8,000.