1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel inakumbuka wanajeshi waliokufa na wahanga

25 Aprili 2023

Israel ipo katika ukumbusho wa wanajeshi waliokufa na wahanga wa mashambulizi ya wanamgambo wakati ambao nchi hiyo inashuhudia mipasuko mikubwa ya kisiasa katika historia yake na mivutano inayoongezeka na Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4QWdF
Israel 75 Jahre Staatsgründung | Mount Herzl, Militärfriedhof
Picha: Menahem Kahana/AFP/Getty Images

Siku ya Ukumbusho ni moja ya nyakati muhimu zaidi katika kalenda ya kitaifa ya Israel, inayotoa heshima kwa askari 24,213 waliouawa vitani na wahanga 4,255 wa mashambulizi.Israel wakati huu inapitia migawanyiko mkubwa kuhusiana na mpango tata wa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wa kuifanyia mabadiliko mapana idara ya mahakama. Mwaka huu, Israel inaadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwake. Aidha, hayo yanafanyika wakati ambapo Israel na Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wanakabiliana katika mojawapo ya machafuko makali zaidi kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo kwa miaka mingi.