Israel imeshinda Lebanon
20 Agosti 2006Matangazo
JERUSELEM:
Mkuu wa majeshi ya Israel ameliambia baraza la mawaziri la israel hii leo kwamba vita nchini Lebanon vilimalizika kwa ushindi wa Israel,lakini sio ushindi wa kuhilikisha kabisa adui.Miongoni mwa mambo mengine, Israel imeteketeza miundombinu ya wanamgambo wa Hizbollah-alisema Jamadari Dan Halutz.
Waziri wa nje wa Uturuki,Abdullah Gul ameelekea leo Israel kuzungumzia mapatano ya kuacha mapigano kati ya Israel na Lebanon na uwezekano wa uturuki wa kuchangia vikosi vya kuhifadhi amani.
Uturuki ikisema hapo kabla kwamba ingechangia vikosi lakini Gul alisema uwanja wa ndege wa Ankara kwamba, Uturuki inatathmini kwanza dhamana za kikosi hicho kabla kupitisha uamuzi.