1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Israel vinapambana na wapiganaji wa Hamas

8 Oktoba 2023

Vikosi vya Israel vinapambana na wapiganaji wa Hamas na kushambulia maeneo ya Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4XGL3
Israel, Ashkelon | Israelische Polizisten im Einsatz
Picha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Vikosi vya Israel vinapambana na wapiganaji wa Hamas na kushambulia maeneo ya Ukanda wa Gaza, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akionya kuhusu vita vya "muda mrefu na vigumu" vilivyo mbele, alivyosema vimesababishwa na mashambulizi makubwa ya kushitukiza ya kundi hilo la wanamgambo wa Palestina.Jeshi la Israel limesema maelfu ya wanajeshi wamepelekwa kupambana na wanamgambo katika maeneo ya kusini mwa jangwa karibu na eneo la pwani, kuwaokoa mateka wa Israel na kisha kulikombowa eneo lote ndani ya masaa 24.Ikiwa ni takribani siku nzima baada ya mamia ya wapiganaji wa Hamas kuvuka kuingia Israel kwa kutumia magari, maboti na miavuli, msemaji wa jeshi Daniel Hagari amesema wataifikia kila jamii hadi watakapomuangamiza kila aliyemuita "gaidi" katika ardhi ya Israel.Mapigano hayo mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa yamesababisha vifo vya zaidi ya Waisraeli 200 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 1,000, na kuacha miili ya raia ikiwa imetapakaa barabarani, huku kwa upande wa Gaza takribani watu 313 wakiuwawa na zaidi ya 1,700 wakiripotiwa kujeruhiwa.